MABINGWA wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, Leo watakuwa kazini kumenyana na Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Chamazi.
Mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema wanatambua ugumu wa kupata matokeo kwa sasa ligi kuu ulivyo ila watatumia vema Uwanja wao wa nyumbani kupata matokeo.
"Tutakuwa nyumbani leo kwenye mchezo wetu dhidi ya Biashara United hivyo hesabu kubwa ni kuona tunafanikiwa kupata pointi tatu muhimu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri.
"Tumefanikiwa kutwaa kombe la Mapinduzi kama tulivyopanga hivyo kwa sasa nguvu zetu ni kwenye Ligi Kuu Bara ili kuleta ushindani," alisema Alando.
0 Comments