Kocha wa zamani wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameibuka na kuwapa hongera Yanga kufuatia usajili wa kiungo, Owen Bonyanga Ituku, kutoka TP Mazembe.
Zahera ameeleza kuwa mchezaji huyo anamjua vizuri na anaamini atawasaidia Yanga kufanya kazi vizuri ndani ya dimba.
“Namjua, ni mchezaji mzuri sana. Kama Yanga wataweza kumtumia watafaidi kwani hana mambo mengi sana anapokuwa uwanjani zaidi ya kuhitaji kupeleka mbele mashambulizi.
“Binafsi naamini safu ya ushambuliaji ya Yanga ikiwa makini inaweza ikapachika mabao mengi kwani huyu mchezaji waliyemsajili sio mchoyo hata kutoa pasi za mwisho, nawatabiria makubwa,” alisema.
Kuhusu Mbelgiji, Luc Eymael, ambaye ndiye sasa kocha mkuu wa kikosi hicho akichukua mikoba yake, Zahera alisema naye ni kocha mzuri kwa sababu amefundisha timu nyingi kubwa zikiwamo za Congo.
“Ni kocha mzuri kama watamtunza kwani amefundisha timu mbalimbali kubwa ikiwamo AS Vita.
"Kocha yeyote akipewa mahitaji yake anaweza kufanya vizuri na kama hatapewa anaweza akaonekana mbaya ndiyo maana nasema wakimpa mahitaji yote atakayoyahitaji watafanikiwa,” alisema.
0 Comments