Kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Kagera Sugar ni salamu kwa kocha mkuu Luc Eymael kuwa ana kazi ya kufanya
Kwa leo Mbelgiji huyo hastahili lawama kwani inafahamika amefanya mazoezi na timu kwa siku mbili tu
Lakini kwa hakika ni moja ya michezo ambayo Yanga imeonyesha kiwango kibovu kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha karibuni
Kwa miaka ya hivi karibuni sikumbuki ni lini Yanga ilifungwa mabao 3-0 au zaidi kwenye ligi
Mchezo wa leo lawama zote wanastahili wachezaji kwani hawakuitendea haki Yanga
Ni jukumu lao kuwapa furaha mashabiki kwa kupata matokeo kila wanaposhuka dimbani
Juhudi zinafanywa na wadhamini pamoja na uongozi wa Yanga kuhakikisha wanapata kila kitu
Nao wanapaswa kutambua hilo kwa kuipigania timu
Msimu uliopita timu haikuwa na hali nzuri kiuchumi lakini wachezaji walijitolea mhanga kupambana
Matokeo haya hayakubaliki ni vyema wakatambua kuwa Yanga sio timu ya kufungwa kizembe
0 Comments