Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael kesho Jumatano ataanza rasmi majukumu ya kuiongoza Yanga katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Kagera Sugar
Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Uhuru
Eymael alianza rasmi kukinoa kikosi cha Yanga jana baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kuwanoa mabingwa hao wa kihistoria
Kocha huyo aliyewahi kuipa AS Vita ubingwa wa ligi kuu ya DR Congo, ametamba kuwa na kikosi chenye wachezaji wenye vipaji
Inaelezwa tayari vibali vyake vya kufanya kazi nchini vimepatikana hivyo huenda kesho akakaa kwenye benchi kuwaongoza vijana wake katika mchezo wake wa kwanza
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store
0 Comments