Nahodha wa Simba John Bocco amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo baada ya kushindwa kutwaa kombe la Mapinduzi jana
Bocco amesema walijiwekea malengo ya kushinda taji hilo lakini haikuwa bahati yao
Aidha Bocco amewapongeza Mtibwa Sugar baada ya kufanikiwa kuibuka mabingwa wa michuano hiyo kufuatia ushindi wao wa bao 1-0
"Tumepoteza mchezo kwa bahati mbaya kwani tulicheza vizuri. Kwenye kipindi cha kwanza na hata cha pili tulitengeneza nafasi lakini tukashindwa kuzitumia. Lakini wapinzani wetu Mtibwa Sugar hawakuwa wabaya nao walicheza vizuri. Hatukufurahishwa na matokeo haya lakini ndio mpira wa miguu ulivyo"
"Tunarejea Dar kuendelea na maandalizi ya michezo ya ligi kuu inayofuata," amesema
Kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar jana, kimeifanya Simba ipoteze mechi ya pili ya fainali ya michuano hiyo kwa msimu wa pili mfululizo
Mwaka jana Simba ilifungwa na Azam Fc mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali
Kocha Sven Vandenbroeck ameingia lawamani kutokana na mabadiliko makubwa ya kikosi aliyofanya
Mashabiki wengine wamewashukia baadhi ya wachezaji kuwa hawakuitendea haki Simba inayowalipa mishahara minono kwani hawakujituma
Ni matokeo ambayo yamepelekea Mwekezaji Mohammed Dewji 'Mo' kujiuzulu nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi hatua ambayo inamfanya ajiondoe kwenye majukumu ya kuihudumia timu na kujikita zaidi katika majukumu ya uwekezaji
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments