Windows

TPLB yasisitiza, mechi ya watani itapigwa January 04



Pamoja na uwepo wa michuano ya kombe la Mapinduzi mwanzoni mwa mwaka, Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara imesisitiza haitafanya mabadiliko ya tarehe ya mchezo wa kwanza wa watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga

Mchezo huo umepangwa kupigwa January 04 2020 kwenye uwanja wa Taifa

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Stephen Mguto amesema wamepeleka mapendekezo kwa waandaaji wa michuano ya kombe la Mapinduzi ili ichezwe kwa mfumo wa mtoano

Hata hivyo amesema vilabu vya Simba na Yanga vitalazimika kurejea nchini kucheza mchezo baina yao January 04

"Tulichofanya sisi ni kuwasiliana na viongozi wa kamati ya maalum inayosimamia michuano ya Mapinduzi, ili watupe maoni yao kuhusu tariba ya ligi hapa Tanzania Bara," amesema Mguto

"Tumeomba michuano ya Mapinduzi iwe ya mtoano ili timu za huku ziweze kucheza mechi zake mara zitakapotoka, lakini kwa Simba na Yanga hata kama zitaingia hatua ya nusu fainali au robo zitatakiwa zirudi Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo huo, hivyo hatutabadilisha"



Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.

Post a Comment

0 Comments