Kocha wa zamani wa Yanga Hans van Pluijm amekiri kuomba nafasi ya kurejea Jangwani kuwanoa mabingwa hao wa kihistoria
Pluijm aliyewahi kuinoa Yanga kwa vipindi viwili tofauti, ndiye kocha wa mwisho kupata mafanikio makubwa Jangwani
Msimu wa 2015/16 aliiwezesha Yanga kutwaa mataji yote ya ndani huku akiipeleka timu hiyo hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho
Pia Pluijm ndiye kocha wa mwisho kuipa ushindi Yanga dhidi Simba mwaka 2015
Kwa sasa yuko mapumziko nchini Ghana ambako ndiko familia yake inaishi
Kilichomsukuma kutaka kurejea Yanga
Pluijm amesema amepokea ujumbe mwingi kutoka kwa wanachama mashabiki wa Yanga wakimuomba arudi kuinoa timu hiyo
Amekiri kutuma maombi wiki tatu zilizopita
Mabadiliko atakayofanya
Pluijm amesema amekiona kikosi cha Yanga na amebaini kina mapungufu makubwa sehemu ya ulinzi na ushambuliaji
"Kama nikirudi Yanga jambo la kwanza nitasajili mshambuliaji mwenye uwezo wa hali juu ambaye atakuwa na jukumu la kufunga mabao"
"Pia nimeona mapungufu kwenye safu ya ulinzi pengine nitahitaji wachezaji wawili au watatu kuimarisha eneo hilo"
Amfagilia Mkwasa
Pluijm ameupongeza uongozi wa Yanga kwa kumteua Charles Mkwasa kuwa kocha wa muda
Mdachi huyo ameeleza kuufahamu uwezo wa Mkwasa na anaamini atafanya vizuri
Mkwasa alikuwa kocha msaidizi wa Yanga wakati Pluijm akiwa kocha mkuu
Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Yanga alikuwa sehemu ya mafanikio ya timu hiyo wakati wa Pluijm
Na bila shaka kocha ambaye Mkwasa anaweza kumpigia 'chapuo' arudi Yanga ni Hans van Pluijm
Kwa habari zaidi Download App ya soka kiganjani kutoka Play Store.
0 Comments