Kumekuwa na taarifa zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii kumuhusu mshambuliaji Sadney Urikhob kuwa ameondoka baada ya kuvunja mkataba wake na Yanga
Hata hivyo jana Yanga ilitoa taarifa kuwa wachezaji wa kigeni wamepewa ruhusu ya kusafiri kwenda kuona familia zao kabla ya timu hiyo kurejea kuendelea na mazoezi siku ya Jumatatu
Hii sio mara ya kwanza Sadney anazushiwa kuondoka Yanga
Kabla ya mchezo dhidi ya KMC iliripotiwa taarifa kama hiyo lakini haikuwa kweli, kwani mchezaji huyo alishiriki mazoezi na hata kucheza mchezo dhidi ya KMC
Lakini pia kuelekea dirisha dogo la usajili wiki ijayo, kuna michakato inafanywa na viongozi wa Yanga katika kuboresha kikosi cha timu hiyo
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema baadhi ya masuala watayaweka wazi wakati wake utakapofika
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments