Windows

MKWASA AWABANIA MOLINGA ,TSHISHIMBI ,SIBOMANA NA BALINYA



Uongozi wa klabu ya Yanga si mchezo kabisa hasa linapokuja suala la kucheza na Simba. Kuelekea mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara klabu ya Yanga imetangaza kuendelea kubaki

kambini kujiandaa na mchezo huo wa ligi .Wachezaji wa Yanga wameambiwa na uongozi: “Hakuna kuvunja kambi, mtabaki hapahapa Dar mpaka mtakapocheza na Simba.”
Hii imetokea siku chache baada ya awali kuaminika kuwa wachezaji hao wakiwa pamoja na David Molinga mwenye mabao manne kwenye ligi, walikuwa wanaweza kuruhusiwa kwenda kukaa na familia zao kipindi hiki ambacho Ligi Kuu ya Tanzania Bara imesimama.
Jana wachezaji wote wa timu hiyo walikuwa wamekusanyika kwenye jengo lao eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam wakisubiri kauli tu ya viongozi ili wasepe zao kula sikukuu za Krismasi, lakini uongozi ukawaambia kuwa hawaendi popote

Baada ya muda kidogo viongozi wa Yanga ambao walikuwa ofi sini hapo walikutana na wachezaji hao ambao juzi walicheza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KMC na kutoka sare ya bao 1-1 na kuwaambia kuwa wanaendelea na kambi.
“Kilichoamuliwa ni kwamba timu itaendelea kuwa kambini hadi mechi ya Simba na Yanga ipite, awali tulifi kiri kuwa tunaweza kuwaruhusu wachezaji waende makwao, lakini tumeona kuwa linaweza kuwa tatizo.“Unaweza kuwaruhusu leo halafu ukikaribia mchezo mchezaji anachelewa kurudi na mwisho tunaweza kupoteza mechi kwa ajili ya uzembe.“Sasa tutakaa hapa, na tutakwenda baadhi ya mikoa kwa ajili ya michezo ya kirafi ki baada ya hapo tutaanza maandalizi rasmi ya kuwavaa Simba Januari 4,” kilisema chanzo cha uhakika.
Baadhi ya wachezaji wa Yanga ambao wapo kambini na walikuwa wanaweza kwenda kula bata makwao ni Papy Tshishimbi, David Molinga, Mrisho Ngassa, Deus Kaseke, Patrick Sibomana na Juma Balinya.

Post a Comment

0 Comments