Klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya baada ya aliyekuwa kocha wao Juma Mwambusi kujiuzulu kufuatia timu hiyo kufanya vibaya katika ligi kuu msimu huu, leo wamemtambulisha kocha mpya.
Mbeya City imemtambulisha rasmi aliyewahi kuwa mchezaji wa zamani wa Simba SC pia na kocha wa zamani wa klabu za Mbao FC na Biashara United Amri Saidi kuwa ndio kocha wao mpya kuchukua nafasi ya Mwambusi.
Amri Said anakuwa kocha wa Mbeya City kama kocha wa mpito katika kipindi cha miezi sita kabla ya bodi ya timu hiyo kufanya maamuzi zaidi.
Timu ya mwisho kuifundisha Amri Said ilikuwa Biashara United ambayo awali aliingia nayo katika msuguano baada ya kuondoka bila kuaga.
0 Comments