Jana baada ya kutambulishwa kuwa kocha msaidizi wa Simba, jioni Selemani Matola aliongoza mazoezi ya mabingwa hao wa nchi yaliyofanyika katika uwanja wao wa Mo Simba Arena
Matola aliyejiunga na Simba akitokea Polisi Tanzania, amesema ameandaa program ya mazoezi ya siku mbili akisubiri ujio wa kocha mkuu
Akizungumza baada ya mazoezi jana, Matola alisema ameanza mazoezi ya kuwaweka fiti wachezaji wake baada ya mapumziko.
Matola alisema programu ambazo zitakuwa zinaendelea katika kikosi chake zitakuwa zote chini yake mpaka kocha mkuu atakapopatikana.
"Kwa hizi siku mbili tatu nitakuwa naiongoza timu mimi, lakini baada ya hapo ratiba zote zitakuwa chini ya kocha mkuu anayekuja," alisema.
Matola ambaye ameichezea klabu hiyo alisema anaiongoza timu hiyo akiamini kwamba atafanya vizuri na ikitokea kuwa vibaya basi ni mipango
Simba inatarajiwa kucheza na Arusha Fc kwenye mchezo wa raundi ya tatu kombe la FA ambao utapigwa Disemba 22 kwenye uwanja wa Uhuru
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments