Windows

Zahera arejea nchini, adai hajamaliziwa malipo



Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amerejea nchini kwa kile alichokieleza kufuatilia malimbikizo ya madai yake

Zahera ambaye ni kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya DR Congo, amesema pia hakuwa amesaini barua ya kuvunjwa kwa mkataba wake

"Hawajamalizia fedha yangu na bado sijasaini barua ya kuvunja mkataba"

"Siwezi kuendelea kukaa huku nikiwa bado sijamalizana na Yanga narudi tena Tanzania kwaajili ya kudai fedha zangu na kusaini hiyo barua ya kuvunja mkataba kama wao wanavyotaka," amesema Zahera



Mcongomani huyo aliondoshwa kwenye nafasi ya kocha mkuu Novemba 05 mwaka huu baada ya Kamati Utendaji ya Yanga kufikia makubaliano ya kuvunja benchi lote la ufundi kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa timu

Tangu wakati huo Yanga inanolewa na Charles Mkwasa ambaye alikabidhiwa kuiongoza timu katika kipindi cha mpito ambacho uongozi utakuwa ukisaka kocha mpya

Mkwasa ameanza vyema majukumu yake kwenye kikosi cha Yanga, huenda akaendelea na majukumu hayo mpaka mwishoni mwa msimu

Post a Comment

0 Comments