Windows

Watu wawili wafariki dunia kwenye ajali ya gari lililobeba mashabiki wa Mwakinyo


Watu wawili wamefariki na wanane wamejeruhiwa katika ajali ya gari la timu ya Coastal Union iliyokuwa imebeba mashabiki wa ngumi waliokuwa wakitoka kutazama pambano la bondia Hassan Mwakinyo dhidi ya Arnel Tinampay lililofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam usiku wa jana.

Ajali hiyo imetokea eneo la Kerege wilayani Bagamoyo, wakati mashabiki hao walipokuwa safarini kurejea jijini Tanga.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Coastal Union Hafidh Kido imewataja waliofariki kuwa ni Ibrahim Omar na Hussen Saleh ambapo uongozi wa Coastal kwa kushirikiana na ndugu zao, wanafanya taratibu za kuwasafirisha kwenda Tanga kwaajili ya maziko.

Hadi sasa miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

"Majeruhi walikuwa wanane, mmoja hali yake ilibadilika amepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, na mwingine tumemkuta hapa anaitwa Aziza, ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kwakaheza mkoani Tanga. Abiria wengine tayari wamerejea Tanga wakiwa pamoja na dereva wa gari letu," imeeleza taarifa ya Kido. .

Katika pambano hilo Mwakinyo ambaye ni mkazi wa Tanga alishinda kwa pointi.

KWA HABARI ZAIDI PAKUA APP YA SOKA KIGANJANI 

Post a Comment

0 Comments