Windows

Samatta mtegoni usiku wa Ulaya

Samatta- mtegoni

Jicho la Genk litamtazama zaidi Samatta kama mkombozi wao kwani, ndiye ameifungia idadi kubwa ya mabao katika mashindano hayo ambapo kati ya manne waliyofunga, nahodha huyo wa Stars amepachika mawili

Genk,Ubelgiji. Mshambuliaji na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta leo atakuwa na jukumu zito la kufufua matumaini ya timu yake ya Genk kushiriki mashindano ya Europa League wakati watakapovaana na FC Salzburg.


Ikiwa inashika mkia katika kundi G na pointi yake moja, Genk inahitajika kupata ushindi dhidi ya Salzburg ikiwa nyumbani leo ili iweke hai matumaini yake ya kucheza hatua ya mtoano ya Europa League.


Timu hiyo ya Ubelgiji haina nafasi ya kucheza hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwani, hata ikiibuka na ushindi katika mechi zake mbili zilizosalia ambazo ni ya leo na ile ya mwisho, itafikisha pointi saba ambazo haziwezi kufikia zile za Napoli inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi nane pamoja na zile za Liverpool inayoongoza ikiwa na pointi tisa.


Kwa upande mwingine mchezo huo unakumbushia mechi ya kwanza katika kundi hilo iliyozikutanisha timu hizo nchini Austria ambako, Genk waliangushiwa kipigo cha mabao 6-2.


Jicho la Genk litamtazama zaidi Samatta kama mkombozi wao kwani, ndiye ameifungia idadi kubwa ya mabao katika mashindano hayo ambapo kati ya manne waliyofunga, nahodha huyo wa Stars amepachika mawili


Mchezo mwingine wa kundi E utakuwa ni baina ya vinara Liverpool watakaoikaribisha Napoli ambayo kama itapoteza basi kocha wake, Carlo Ancelotti kibarua kinaweza kuota nyasi wakati katika kundi F, Barcelona itaikaribisha Borussia Dortmund wakati Slavia Plague itaumana na Inter Milan. Zenit St. Petersburg itakuwa nyumbani kuikabili Lyon na Leipzig itacheza na Benfica zikiwa ni mechi za kundi G. Huko katika kundi H Valencia itakuwa nyumbani kuikaribisha Chelsea ya Frank Lampard wakati Lille itaikaribisha Ajax.

Post a Comment

0 Comments