Windows

Mshambuliaji wa Tanzania asaka namba ndani ya TP Mazembe




Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayecheza TP Mazembe ya DR Congo, Eliud Ambokile anasema bado anapigana kuhakikisha anatoboa kucheza kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Ambokile anasema bado hajapata nafasi ya kutosha kucheza kwenye kikosi cha Mazembe lakini anafarijika kuendelea kufunga kwenye mechi za kirafiki.

“Changamoto ni kubwa inahitaji kuwa mvumilivu kwa sababu hakuna kazi rahis siku zote. Ushindani ni mkubwa sana ndio maana unaona kupata nafasi imekuwa ngumu lakini naimani mbele itapatikana kikubwa kuzidi kukaza bila kukata tamaa maana tumeshawakuta watu kwenye mfumo kwa hiyo lazima tuheshimu tuliowakuta.”

“Nimecheza mechi moja ya ligi lakini sikufanikiwa kufunga, mechi nyingine tatu nilikaa kwenye benchi.”

Hadi Mshambuliaji huyo amefunga magoli sita lakini magoli yote amefunga kwenye mechi za kirafiki alizocheza.



Post a Comment

0 Comments