Windows

Ajib, Kahata wachuana kutengeneza mabao Simba





Viungo wa Simba Francis Kahata, Ibrahim Ajibu wameingia kwenye vita mpya ya kumsaka mkali wa pasi za mwisho baada ya wote mpaka sasa kufikisha jumla ya pasi tatu ndani ya kikosi cha Simba.

Mbabe wa asisti ndani ya Ligi Kuu Bara msimu uliopita alikuwa ni Ajibu ambapo alipokuwa Yanga alitoa jumla ya asisti 17 ila mpaka sasa ametoa jumla ya asisti tatu sawa na Kahata.

Asisti yake ya kwanza aliitoa kwa Miraji wakati Simba ikishinda mabao 2-0 mbele ya Biashara United na mbili alitoa kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City wakati Simba ikishinda mabao 4-0 asisti zilizofanyiwa kazi na Clatous Chama na Sharaf Shiboub.



Kwa upande wa Kahata alianza kumpa Meddie Kagere mbele ya Azam FC wakati Simba ikishinda bao 1-0 na mbili alitoa kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shoting wakati Simba ikishinda mabao 3-0 zilitendewa haki na Sheva pamoja na Tairone Santos



Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.

Post a Comment

0 Comments