

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, juzi Jumamosi alikutana na balaa kutoka kwa wachezaji wa kikosi hicho baada ya kumpaka keki usoni na kummwagia maji ikiwa ni siku ya kumbukumbu yake ya kuzaliwa.
Zahera ambaye kesho Jumanne atakiongoza kikosi hicho kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbao FC alikutana na balaa hilo wakati akisherehekea kutimiza miaka 57 tangu aingie duniani.
Tukio hilo lilifanyika juzi usiku wakati kikosi hicho kikiwa katika Hoteli ya Mipa ambapo wameweka kambi kwa ajili ya mechi hiyo na Mbao FC ya Mwanza na mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika watakaocheza na Pyramids FC ya Misri.
Mmoja wa wachezaji wa Yanga aliliambia Championi Jumatatu, kuwa: “Ilikuwa sehemu ya furaha tu na kusherehekea siku hiyo ya kuzaliwa ya kocha Zahera ndiyo mambo yote hayo yakatokea, tulimpaka keki lakini pia tukammwagia maji maana si tunajua tena birthday za siku hizi.”
Rekodi zinaonyesha kuwa Zahera ambaye ana uraia wa nchi mbili DR Congo na Ufaransa amezaliwa Oktoba 19, 1962 ambapo juzi Jumamosi alisherehekea kutimiza miaka 57.
SAID ALLY, Dar es Salaam
The post Zahera Achafuliwa Uso Mwanza appeared first on Global Publishers.



0 Comments