Windows

Global FC Yapanga Kuichakaza Dawasa

BAADA ya kutoka sare katika michezo miwili ya ligi ya makampuni ya Umma na mashirika binafsi,timu ya Global FC leo imepania kuondoka na ushindi katika mchezo wao dhidi ya Dawasa FC,katika uwanja wa Gymkhana jijini Dar.

Global FC katika michezo yote miwili ya ligi hiyo ilitoka sare ya bila kufungana ambapo mchezo wa kwanza ilicheza na TBC FC na mchezo wa pili ilicheza na Twiga FC.

 

Nahodha msaidizi wa timu hiyo, Omary Mdose ‘Hazard’ ameliambia Spoti Xtra kuwa baada ya sare ya michezo miwili iliyopita sasa ni muda wa kupata ushindi na watafanya hivyo dhidi ya Dawasa.

 

“Tumepata sare katika michezo miwili ,ili tujiweke katika nafasi nzuri inatubidi tupate ushindi na ushindi huo tutaupata kwenye mchezo wetu dhidi ya Dawasa leo hii,” alisema Nahodha huyo.

The post Global FC Yapanga Kuichakaza Dawasa appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments