


MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, ameipa onyo kali Klabu ya Yanga na kuitaka kutoomba tena kusogezwa mbele kwa mchezo wao wowote wa ligi kuu pasipokuwa na sababu za msingi. Wambura ametoa kauli hiyo baada ya Bodi ya Ligi kukubali ombi la Yanga la kusogeza mbele mchezo wa ligi.
BAADA ya kuondolewa kwenye raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameanika mipango yake mipya kuelekea Kombe la Shirikisho Afrika. Yanga itashiriki kombe hilo baada ya kuondolewa na Zesco United ya Zambia katika baada ya kufungwa wikiendi iliyopita mabao 2-1 mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa na hivyo kutolewa kwa mabao 3-2.

Yanga hivi sasa inasubiria kuchezwa kwa droo ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) itakayochezeshwa wiki ijayo ili kujua atacheza na nani. Akizungumza na Championi Jumatano, Zahera alisema amejifunza mengi katika ushiriki wa michuano hiyo na kitu walichokosea ni kucheza bila mipango ya ushindi wa mabao mengi nyumbani.
Zahera alisema ushindi wa mabao mengi kuanzia matatu wa nyumbani ni mtaji mkubwa watakapokwenda ugenini, hivyo amejipanga kuhakikisha makosa waliyoyafanya kwenye Ligi ya Mabingwa hawayafanyi kwenye shirikisho.
“Hili kuwa na uhakika wa kutinga makundi tunahitaji kufunga mabao mengi nyumbani, tutaanzia hapa kabla ya kwenda kurudiana na wapinzani kwao.

“Huo ndiyo mpango mkakati niliopanga kuuanza katika Shirikisho, kwani tayari benchi la ufundi pamoja na wachezaji tumejifunza hilo, unapokuwa na mtaji mkubwa wa mabao ukiwa nyumbani, basi ni rahisi kufuzu ugenini kutokana na presha itakayokuwepo kwa wapinzani wetu.
“KiuKweli tulikuwa na changamoto kubwa kwenye safu yetu ya ushambuliaji ambayo ilikosa umakini katika umaliziaji kutokana na kutengenezewa nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia, lakini sasa nadhani tumeanza kuwa vizuri. “Hatupaswi kurudia makosa tuliyofanya Ligi ya Mabingwa, tunahitaji kufunga mabao zaidi ya mawili tukiwa nyumbani ili kupunguza presha ya mchezo wa ugenini na hilo linawekana kwetu,” alisema Zahera.
kuu dhidi ya Polisi Tanzania uliopangwa kuchezwa leo Jumatano, lakini sasa utachezwa kesho Alhamisi. Kisha mchezo ujao watakipiga dhidi ya Coastal Union Jumapili ya wiki hii. Michezo hiyo yote itachezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar. Akizungumza na Championi Jumatano Wambura, alisema:
“Tumekubaliana na Yanga juu ya ombi lao na sasa michezo yao yote miwili itachezwa wiki hii, wataanza na Polisi Tanzania Alhamisi, kisha mchezo mwingine watalazimika kucheza tarehe 6 ambayo itakuwa Jumapili dhidi ya Coastal Union.
“Sambamba na hilo, tunatoa onyo kwa Klabu ya Yanga na klabu nyingine yoyote kuacha hii tabia ya kuomba michezo yao isogezwe mbele bila sababu za msingi kwani hii tabia ikiendelea itatuletea mkanganyiko huko mbele,” alisema Wambura. Yanga walipeleka ombi Bodi ya Ligi ya kutaka mchezo wao na Polisi Tanzania kusogezwa mbele kwa kile walichodai timu yao imeshindwa kuwasili Dar kwa wakati ikitokea Zambia ilikokuwa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika
The post Bodi ya Ligi yaipa Onyo kali Yanga appeared first on Global Publishers.



0 Comments