


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amesema kuwa, mshambuliaji wake, Miraj Athuman maarufu kama Sheva amechukua mikoba ya Emmanuel Okwi katika kuifanya timu hiyo kuendelea kuwa bora kwenye Ligi Kuu Bara.
Kauli ya Aussems raia wa Ubelgiji imekuja ikiwa ni baada ya Sheva aliyejiunga na timu hiyo msimu huu kuanza na moto wa hatari.
Katika mechi nne za Ligi Kuu Bara alizocheza, Sheva amefunga mabao matatu kati ya kumi ambayo yamefungwa na timu hiyo hadi sasa ambayo inaongoza ligi ikiwa na pointi 12.
Awali, wakati Okwi anaachana na Simba mwishoni mwa msimu uliopita na kutimkia Misri, ilionekana timu hiyo itayumba, lakini Aussems amesema Sheva ameiweka sawa.
Akizungumzia hilo, Aussems amesema: “Siwezi kuumia kuondoka kwa Okwi kwa kuwa kama mchezaji kuondoka kwenye timu ni jambo la kawaida.
“Ukiangalia hivi sasa, Sheva ameweza kufanikiwa kwa kiasi fulani katika kuifanya Simba iwepo hapa ilipo sasa kutokana na mipango yetu.
“Naamini kama ataendelea kwa kasi na uwezo ambao yupo nao kwa sasa, basi kuna nafasi kubwa ya yeye kufanya vizuri na kuwa mchezaji mkubwa hapo baadaye.”
The post Aussems: Sheva ndiye mrithi wa Okwi appeared first on Global Publishers.



0 Comments