HATIMAYE ule mpambano wa karne kati ya timu ya Waliooa FC dhidi ya Wasiooa FC zote za Makampuni ya Global Group, umepigwa jana Ijumaa, Septemba 6, 2019, katika Uwanja wa CCM, Sinza jijini Dar es Salaam huku Waliooa FC wakiibuka na ushindi wa bao 2-1.
Mechi hiyo iliyokuwa na ushindani wa aina yake ilianza majira ya saa 10:00 huku Timu zote zikiwa zimekamiana na kila mmoja akiwa na uchu wa kuchungulia nyavu za mwenzake.
Wasiooa FC walianza kwa kasi huku wakilisakama lango la Waliooa FC mara kwa mara lakini kwa umaridadi wa kipa wa Wasiooa FC, ilikuwa ngumu kwani alikuwa akiokoa michomo kama de Gea vile.
Mambo yalianza kubadilika kuanzia dakika ya 20, ambapo Waliooa FC wali-gain momentum na kurejea mchezoni rasmi hali iliyowashangaza mashabiki wengi wa Timu hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wao, Eric Shigongo, walilisakama lango la Wasiooa FC kama nyuki na kunako dakika ya 35, Wasiooa FC wakafanikiwa kupata bao la kwanza kupitia kwa Hamisi bao ambalo lilidumu kwa kipindi chote cha kwanza.
Kipindi cha pili hali ilikuwa vilevile, Wasiooa FC walifanya mabadiliko wakimtoa Mbrazil, Santosh, Amran Kaima na Saleh Ally Jembe, na nafasi zao kuchukuliwa na Ally Mbetu, Borry Mbaraka na Deo, mabadiliko ambayo yaliiongezea nguvu mpya timu hiyo.
Dakika ya 65, Wasiooa FC walifanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa Wilbert Molandi ‘Momo’ baada ya kutokea piga nikupige iliyosababishwa na mpira wa adhabu langoni mwa Wasiooa FC na kujihakikishia ushindi huo mnono na wa kihistoria.
Dakika ya 70, Wasiooa FC walizinduka kutoka usingizi wa pono waliokuwa wamelala, na kuanza kulisakama tena lango la Waliooa FC. Dakika ya 84 walifanikiwa kupata mpira wa adhabu baada ya mchezaji wao Abdul kufanyiwa madhambi nje ya 18.
Mpira huo wa adhabu ulipigwa na Said Omary na kuzama moja kwa moja wavuni hivyo kuwaandikia Wasiooa FC bao la kufutia machozi, mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa, Waliooa FC 2-1 Waliooa FC.
Timu ya Wasiooa FC ipo chini ya udhamini mnono wa Kessy Marketing Agency Kessy Marketing Agency na Waliooa FC imedhaniniwa na Saleh Jembe Blog Saleh Jembe Facts.
Na Edwin Lindege.
The post Waliooa FC Waitungua Wasiooa FC – Pichaz appeared first on Global Publishers.
0 Comments