Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania kimesema kimejindaa vyema kuwakabili Sudan katika mchezo wao wa hatua ya kwanza ya kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya ( CHAN) 2020 Nchini Cameroon.
Akizungumza na waandishi wa habari Kocha Mkuu wa Tanzania Juma Mgunda amesema kuwa timu yake imejiandaa vizuri kinachotakiwa watanzania kuujaza uwanja wa Taifa kuishangilia timu ili ifanye vizuri.
Aidha nahodha wa Tanzania Juma Kaseja amesema wachezaji wote wana morali ya kupata matokeo katika mechi hiyo huku akiwatoa wasiwasi watanzania kuipiga Sudan.
Kwa upande wake Kocha wa Sudan pamoja na nahodha wake wamesema wanafahamu itakua mechi ngumu kutokana na kikosi cha Tanzania kuwa kizuri lakini lengo lao kupata matokeo wakiwa ugenini.
Mechi itakuwa ya kwanza katika hatua hiyo kuwania kufuzu kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa Ligi za Ndani CHAN.
Kumbuka Stars inakutana na Sudan kesho jumapili baada ya kazi kubwa ya kuwatoa Kenya.
The post Video: Walichosema Kocha wa Taifa Stars na SUDAN Mechi Ya Kesho appeared first on Global Publishers.
0 Comments