MZEE Ibrahim Akilimali, amekiri kwamba anateseka na anahitaji michango kutoka kwa watu ili kulipa deni analodaiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, baada ya kufanyiwa operesheni ndogo tumboni.
Akilimali ambaye ni mmoja wa vigogo wa Baraza la Wazee wa Yanga aliyeendesha harakati katika masuala mbalimbali klabuni hapo, anasumbuliwa pia na ugonjwa wa kisukari alionao kwa muda mrefu.
Anasema kwamba anadaiwa Shilingi za Kitanzania 369,000 pale Muhimbili. Akizungumza na Spoti Xtra, Akilimali alisema; “Hali yangu si mbaya kwa sasa, naendelea vizuri lakini nadaiwa shilingi 369,000 na mpaka sasa sijalipa chochote, naomba kama wadau wataguswa na kuumwa kwangu wanisaidie walau hata kidogo.
“Inabidi nianze kulipa walau kidogokidogo maana sasa nikienda hospitali kwa ratiba niliyopewa na daktari nitakuwa sifanyiwi huduma maana sijalipa chochote, hata wao wamenitaka nilipe la sivyo sitahudumiwa,” alisema Akilimali na kuomba watakaoguswa wamtumie au kuwasiliana nae kwenye namba 0658668819 na jina ni IBRAHIM OMARY AKILIMALI
The post Mzee Akilimali: Nateseka, Niokoeni appeared first on Global Publishers.
0 Comments