

VITA ya magolikipa wawili wa KMC ambao wote wanazitumikia timu zao za Taifa jana ilimalizika Uwanja wa Taifa kwa mmoja (Juma Kaseja ambaye ni Mtanzania) kuibuka mbabe baada ya kuipeleka timu yake hatua ya makundi.
Kaseja ambaye pia ni mlinda mlango wa Klabu ya KMC na Jonathan Nahimana wa Timu ya Taifa ya Burundi ambaye aliingia akichukua nafasi ya Justin Ndikumana dakika ya 119, kwenye mchezo huo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar, Kaseja kuokoa penalti moja na mbili wapigaji wa Burundi kukosa.
Akizungumza baada ya kuokoa mikwaju miwili ya penati na kuipaisha Stars, Kaseja amesema hajawahi kufundishwa jinsi ya kudaka penati lakini kikubwa amekuwa akifanya mazoezi na zaidi ni kipaji alichobarikiwa kuwa nacho ndicho kinamfanya awe hivyo.
Kwa upande wa Tanzania mfunguzi alikuwa ni Erasto Nyoni kisha Himid Mao na msumari wa mwisho ukapachikwa na Gadiel Michael.
Tanzania inasonga mbele kwenye hatua ya makundi Kwa Ushindi wa penalti 3-0 baada ya dakika 120 kukamilika Kwa kufungana bao 1-1. Ikumbukwe kuwa mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Burundi timu zote zilitoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1.
MSIKIE KASEJA AKIFUNGUKA
The post Kaseja: Sijawahi Kufundishwa Kudaka Penalti – Video appeared first on Global Publishers.



0 Comments