

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema ziara ya kikosi hicho katika mikoa ya Kanda ya kaskazini haina manufaa yoyote.
Zahera amefunguka kwa kusema kuwa ziara hiyo haina manufaa hasa katika kipindi hiki ambacho kikosi hicho cha Yanga kinakabiliwa na mchezo marudiano wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana.
"Tuna mchezo mgumu na muhimu wa marudiano dhidi ya Township Rollers.
"Nahitaji muda kuiandaa timu lakini tunakuja kupoteza muda huku Moshi na Arusha.
"Tumecheza na Polisi kisha AFC katika viwanja vibovu hakuna jambo la maana tulilofaidika nalo hii ziara tungeweza kuifanya muda mwingine sio huu" amesema Zahera baada ya mchezo wa jana dhidi ya AFC Leopards"




0 Comments