

FREDRICK Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kikosi kinajipanga kwa ajili ya mchezo wa marudio wa kimataifa dhidi ya Township Rollers ya Botswana.
Mwakalebela amesema Yanga imeamua kuweka kambi mkoani Kilimanjaro ili kujiandaa na mchezo huo ambao utakaopigwa Agosti 23 nchini Botswana.
Mwakalebela amesema wakiwa kambini, watacheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania (Agosti 16) na AFC Leopards (Agosti 18)
"Kocha Mkuu Mwinyi Zahera amewasema kuwa wachezaji wote wana ari kubwa kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Rollers hivyo matumaini ya kupata ushindi ni makubwa," amesema.




0 Comments