Kikosi cha Yanga kinaelekea mkoani Arusha kuweka kambi ya maandalizi ya mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers
Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa, Yanga inahitaji kushinda Botswana au hata sare ya kuanzia mabao mawili itawabeba hatua inayofuata
Hali hiyo inaufanya mchezo huo uwe wa kufa na kupona kwa mabingwa hao wa kihistoria
Kutolewa raundi ya kwanza kwenye michuano hiyo ni jambo amalo halitawafurahisha mashabiki wa timu hiyo ambao wengi wamerejesha imani baada ya kikosi kusukwa upya
Yanga itaelekea mkoani Arusha ikiwa na majembe yake yote wakiwemo Kelvin Yondani, Juma Abdul na Andrew Vicent ambao hawakuwa kikosini
Maproo kupata vibali
Habari njema zaidi ni kuwa kwenye mchezo wa marudiano huko Botswana Yanga itakuwa na uhakika wa kuwatumia nyota wake Farouq Shikalo, Mustapha Suleyman na David Molinga ambao walikosa mchezo wa kwanza kutokana na kukosa vibali
Kocha Mwinyi Zahera amesema wachezaji hao watakiongezea nguvu kikosi chao kwenye mchezo wa marudiano
Ikiwa Arusha Yanga itacheza michezo miwili ya kirafiki; August 16 itacheza na Polisi Tanzania mkoani Kilimanjaro na August 18 itacheza na AFC Leopards
0 Comments