Windows

Wamiliki wa Mabenki nchini waanza kutekeleza agizo la Waziri Mkuu


Wamiliki wa Mabenki nchini (TBA) wametekeleza agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kuwataka kutoa mikopo kwa wanunuzi wa pamba nchini.

Majaliwa alitoa wito huo mwishoni mwa wiki mwishoni mwa wiki alipozungumza na wakuu wa mikoa inayolima pamba ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera, Geita, Tabora na Singida pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmaji Nsekela ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabenki (TBA).

Majaliwa alisema mikopo hiyo itawasaidia wanunuzi wa pamba katika kukamilisha taratibu za kununua zao hilo kutoka kwa wakulima.

Akizungumza, Nsekela alisema agizo hilo la Waziri Mkuu limeshaanza kutekelezwa katika mikoa yote inayolimwa pamba hapa nchini.

Nsekala alisema japo mikopo hiyo ilikuwa ikitolewa tangu zamani, lakini kauli ya Waziri Mkuu imeongeza msisitizo kwa mabenki kuhakikisha yanatoa huduma hiyo kwa wanunuzi kwa haraka.

Alisema mabenki ambayo yalikuwa hayafanyi hivyo au yaliyokuwa yanasuasua katika hilo, ndiyo hasa yaliyokuwa yanalengwa.

Majaliwa aliagiza kuwa ununuzi wa pamba utakapoanza kipaumbele kiende kwa pamba iliyokusanywa tayari ili isombwe na kutoa nafasi kwa pamba mpya kuendelea kununuliwa na kupelekwa kwenye maghala.

Post a Comment

0 Comments