UONGOZI wa Yanga umesema kuwa ni lazima madai ya wachezaji wanaoidai timu hiyo yafanyiwe kazi kabla ya kurejeshwa ndani ya kikosi hicho.
Juma Abdul pamoja na Andrew Vincent 'Dante' hawajajiunga na timu kutokana na kudai stahiki zao huku habari zikieleza kuwa wamesimamishwa moja kwa moja ndani ya klabu hiyo.
Mwinyi Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ameongea na wachezaji hao pamoja na viongozi ili kufikia muafaka mzuri kabka yao kurejea kikosini.
"Juma Abdul na Dante, hawa wana kesi ya msingi na wanachokidai ni haki yao lazima walipwe, nimewaambia viongozi kwamba wafanye juu chini hawa wachezaji wapewe stahiki zao ili wajiunge na timu.
"Kuhusu Yoondani yeye anaruhusa maalumu hivyo timu ikirejea ataungana nayo kwani hajagoma.
"Taarifa zao ninanzo na ninatambua kwamba wana kitu cha msingi hivyo imani yangu ni kwamba muda si mrefu mambo yatakaa sawa na wataungana na wenzao kuendelea kupambana," amesema.

0 Comments