Windows

Tutajiandaa kushinda mchezo wa pili - Sibomana




Winga wa Yanga Patrick Sibomana (PS) amesema licha ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Township Rollers, wanayo nafasi ya kupata matokeo ugenini

Sibomana alifunga bao pekee la Yanga kwa mkwaju wa penati kwenye dakika ya 86

Hata hivyo Mnyarwanda huyo alikosa mkwaju wa kwanza wa penati kwenye kipindi cha kwanza

"Sio tatizo kukosa penati, mambo haya yanatokea kwenye mpira wa miguu. Lakini nilichukua jukumu la kupiga penati ya pili kwa sababu nilikuwa najiamini"

"Tutajiandaa kwa ajili ya mchezo wa marudiano, tunahitaji kushinda"

Post a Comment

0 Comments