Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema walifanya makosa kuruhusu bao la mapema ambapo sasa watalazimika kwenda kupata matokeo ugenini
Yanga imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Township Rollers kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa uliopigwa uwanja wa Taifa
"Unapocheza nyumbani kwenye michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho haupaswi kuruhusu bao, sisi tumeruhusu"
"Tutakuwa na kazi ya kufanya ugenini kwani nasi tutapaswa kufunga"
"Lakini tunao uwezo wa kufunga ugenini hata mabao mawili," amesema
"Wapinzani wetu sio wabaya, walicheza vizuri kwenye kipindi cha kwanza lakini nasi tukasahihisha makosa yetu na kuwa imara kwenye kipindi cha pili"
Licha ya matokeo hayo, Yanga ilionyesha kandanda safi, kama washambuliaji wake wangekuwa na mipango mizuri, pengine wangeweza kuibuka na ushindi mnono
Mabingwa hao wa kihistoria walisawazisha bao kwenye dakika ya 86 kupitia mkwaju wa penati uliowekwa kimiani na Patrick Sibomana
Sibomana pia alikosa mkwaju wa penati kwenye kipindi cha kwanza
0 Comments