Windows

SERIKALI YAJIVUNIA TIMU NNE KIMATAIFA


PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa kwa sasa Serikali inajivunia uwepo wa timu nne ambazo zinawakilisha nchi kwenye michuano ya Kimataifa ndani ya Afrika.

Tanzania inawakilishwa na timu nne kwenye michuano ya kimataifa ambazo ni Simba na Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Azam FC pamoja na KMC zinapeperusha Bendera kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Makonda amesema:"Kwa sasa kuna kitu ambacho kinaonekana hapo baadaye hasa ndani ya Tanzania kwenye michuano ya kimataifa hasa ukizingatia kwamba tuna timu nne ambazo zinaipeperusha Bendera kimataifa.

"Timu zote nne ninazipa sapoti kwani siku zote huwa ninasema mimi ni mpenzi wa Yanga, shabiki wa Azam, mkerereketwa wa KMC na mwanachama wa Simba," amesema.

 Kwenye kilele cha Simba day jana, Makonda alikuwa miongoni mwa wageni maalumu ambapo alikaa kwenye siti za wachezaji ambao huwa wanakaa benchi.

Post a Comment

0 Comments