KLABU ya Ligi Kuu ya England maarufu kwa jina la Premier League, zimetumia takribani pauni bilioni 1.4 (Sh trilioni 3.8) kwa ajili ya kufanua usajili katika dirisha lililofungwa Alhamisi ya wiki iliyopita.
Kiasi hicho cha fedha kina ongezeko kubwa la pauni milioni 158 zaidi ya kile kilichotumika msimu uliopita, kwa jumla fedha hizo kwa thamani ya fedha za kitanzania ni ma-trilioni ya shilingi.
Tayari ligi hiyo imeshaanza kwa kasi na moto umeonekana kuwa mkali kwa Manchester City, Manchester United, Liverpool ambazo zimeanza kwa kishindo. Lakini wakati ligi ikitarajiwa kuendelea wikiendi hii, tujikumbushe kidogo kilichotokea wakati wa kujiandaa na msimu huu wa 2019/20 hasa katika usajili ambao ulifungwa Agosti 8, 2019.
Beki Harry Maguire alikuwa ndiye mchezaji ghali zaidi katika usajili huo mkubwa kutokana na kusajiliwa na Manchester United akitokea Leicester City kwa pauni 80m.
Arsenal ilifuatia kwa kumwaga pauni 72m kwa Lille ili kumsajili mshambuliaji Nicolas Pepe, dili nyingine kubwa zilizotamba ni usajili wa Tan-guay Ndombele (pauni 63m kutua Tottenham) na Manchester City kuwasajili Rodri
(pauni 62.5m) na Joao Cancelo (pauni 60m).
KLABU ZILIZOMWAGA MPUNGA MWINGI
Manchester United inashika nafasi ya kwanza kwa kutumia pauni 148m kusajili huku Maguire akichukua sehemu kubwa ya fedha za usajili huo. Wengine ni beki Aaron WanBissaka (pauni 50m kutoka Crystal Palace) na Daniel James (pauni 18m kutoka Swansea City).
Ajabu ni kuwa timu ambayo ndiyo kwanza imepanda daraja ya Aston Villa inaikaribia United katika kumwaga fedha, hiyo yote ni katika kuonyesha kuwa inataka kufanya kweli. Licha ya kuanza msimu vibaya kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Tottenham lakini ilitoa ushindani mkali katika mchezo wao wa kwanza wa Premier League.
Imetumia pauni 144.5m kufanya usajili wa wachezaji 12, walioongoza kusainiwa kwa dau kubwa ni Tyrone Mings (pauni 26.5m), Wesley (pauni 22m), Matt Targett (pauni 17m) na Douglas Luiz (pauni 15m). Arsenal ambayo awali ilionekana kama haina mpango wa kumwaga fedha zaidi ya pauni 45m katika usajili, ilibadili gia na kutoa kitita kikubwa cha fedha kwa ajili ya kusajili.
Imetumia pauni 138m kwa jumla, kwani mbali na Pepe, wengine waliosajiliwa ni William Saliba (pauni 27m, ambaye hata hivyo ametolewa kwa mkopo kwenda St Etienne), Kieran Tierney (pauni 25m), David Luiz (pauni 8m), Gabriel Martinelli (pauni 6m) na Dani Ceballos (pauni 6m).
Manchester City imewekeza pauni 134.8m, zaidi ni katika ulinzi, imemsajili kiungo mkabaji Rodri (pauni 62.5m) na beki wa pembeni Joao Cancelo (pauni 60m), mbali na hao wengine ni Zackary Steff en (pauni 7m) na Angelino Jose Angel (pauni 5.3m).
Everton inaendelea kupambana kufanya kikosi chake kuwa bora kila msimu, kwani imetumia pauni 118.5m kusajili huku gumzo kubwa ikiwa ni usajili wa Alex Iwobi kutoka Arsenal kwa pauni pauni 28m kutoka Arsenal. Mnigeria huyo alisajiliwa siku ya mwisho ya dirisha la usajili na kuungana na Moise Kean (pauni 27.5m), JeanPhillippe Gbamin (pauni 25m), Andre Gomes (pauni 22m) na Fabian Delph (pauni 9m).
Tottenham ambayo imekuwa na kawaida ya kutotumia fedha nyingi kusajili imewshangaza wengi kwa usajili wa mbwembwe wa pauni 100m. Iliwasajili Ryan Sessegnon kutoka Fulham kwa pauni 30m, Tanguy Ndombele (pauni 55m) na chipukizi Jack Clarke (pauni 8.5m).
Kwa hali hiyo tayari presha imeanza kuwa kubwa kwa kocha Mauricio Pochettino kuhakikisha timu yake inapigania mataji. Chelsea, licha ya kuwa imefungiwa lakini ilifanikiwa kufanya usajili mapema kwa kumshusha Mateo Kovacic kutoka Real Madrid kwa pauni 40m.
Kovacicamesajiliwa baada ya msimu uliopita kuichezea Chelsea kwa mkopo. Leicester City wametumia pauni 91m, wengine wanaofuata ni West Ham msimu uliopita, kwa ghali zaidi katika usajili huo Wengine ni beki Aaron WanBissaka (pauni 50m kutoka Crystal Palace) na Daniel James (pauni 18m kutoka Swansea City).
Ambayo ndiyo kwanza imepanda daraja ya Aston Villa inaikaribia United katika kumwaga fedha, hiyo yote ni katika kuonyesha kuwa inataka kufanya kweli. kuanza msimu vibaya kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Tottenham lakini kuwa mkali mkubwa kutokana na kusajiliwa na Manchester United akitokea Leicester City kwa pauni 80m.
Kumwaga pauni 72m kwa Lille ili kumsajili mshambuliaji Nicolas Pepe, dili nyingine kubwa zilizotamba ni usajili wa Tan-guay Ndombele (pauni 63m kutua Tottenham) na (pauni 78m), Newcastle, Wolves (wote pauni 65m), Brighton (pauni 58.5m), Southampton (pauni 50m), Bournemouth (pauni 45.7m) na Watford (pauni 45.5m).
Norwich City ambao wamepanda daraja, wametumia pauni 1.1m, vigogo Liverpool (pauni 4.4m), Crystal Palace (pauni 11m), Burnley (pauni 15m) na Sheffi eld United (pauni 43m).
MAUZO YA WACHEZAJI
Kwa jumla mauzo ya wachezaji katika Premier League kwenye dirisha hilo la usajili ni pauni 806.5m kutoka katika wachezaji 183 waliouzwa rasmi, ikiwa ni ongezeko la pauni 359m kutoka katika dirisha la msimu uliopita.
Chelsea inaongoza kwa kupokea mkwanja mrefu, imeingiza pauni 213.2m, hasa ni baada ya kumuuza Eden Hazard kwenda Real Madrid kwa pauni 130m na Alvaro Morata kwenda Atletico Madrid kwa pauni 58.3m. Kwa jumla Eden Hazard ndiye mchezaji ghali zaidi kwa walioingia na kutoka katika Premier League msimu huu.
Leicester City wanafuatia kwa kuingiza mkwanja mrefu kutokana na mauzo ya Maguire, Manchester United nao wameingiza pauni 74m, Everton (pauni 60m), Manchester City (pauni 58.1m), Arsenal (pauni 55.5m), Crystal Palace (pauni 50m) na Bournemouth (pauni 36.5m).
West Ham (pauni 33.25m), Newcastle (pauni 31.7m), Tottenham (pauni 29.7m), Liverpool (pauni 28.82m), Southampton (pauni 26m), Watford (pauni 18.2m), Burnley (pauni 8.5m) na Wolves (pauni 3m)
EVERTON WACHEZAJI 34 KUINGIA, KUTOKA
Klabu ya Everton imekuwa ndiyo iliyohusika na usajili wa wachezaji wengi kwa jumla katika walioingia na kutoka, hapa ni hadi wale waliotolewa kwa mkopo.
Jumla ya wachezaji 34 wamehusika katika mchakato wao huo, wameruhusu wachezaji 17 kuondoka rasmi kwa mikataba yao kuvunjwa, kumalizika au kuuzwa, pia wameruhusu wachezaji 10 wao kuondoka kwa mkopo.
Waliosajiliwa rasmi kikosini hapo ni saba ambao ni André Gomes kutoka Barcelona, Sebastian Kristensen (Lyngby), Jonas Lössl (Huddersfi eld Town), Fabian Delph (Manchester City), JeanPhilippe Gbamin (Mainz 05), Moise Kean (Juventus) na Alex Iwobi (Arsenal).
Aston Villa imeshika nafasi ya kwanza katika orodha ya timu ambazo zimefanya usajili wa wachezaji wengi kuliko klabu nyingine zote. Villa imesajili wachezaji 12 ikifuatiwa na Sheffi eld United iliyosajili wachezaji nane na wawili wa mkopo, wanaofuata ni Wolves waliosajili wachezaji tisa na mmoja wa mkopo.
The post Premier League Usajili wa Sh Trilioni 3.8 appeared first on Global Publishers.
0 Comments