Mahudhurio hafifu ya mashabiki kwenye mchezo wa jana dhidi ya Township Rollers yameibua mjadala mkali miongoni mwa mashabiki wa Yanga
Pamoja na kazi nzuri inayofanywa na Dismas Ten ambaye ni Afisa Habari na sasa akikaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Wanayanga wengi wanadhani kitengo hicho cha habari na uhamasishaji kinahitaji kuongezewa nguvu kwa kuwekwa mtu ambaye anaweza kuwa na uwezo wa 'amsha-amsha'
Yanga ya sasa inajiendesha 'kiulaya' sana, lakini kwa bahati mbaya ni utamaduni ambao haujazoeleka hapa kwetu
Miaka ya nyuma Yanga ilivyokuwa na Mh Jerry Muro (sasa DC wa Arumeru), mashabiki walikuwa wakienda uwanjani
Na ndio kilikuwa kipindi ambacho Yanga ilikuwa imetawala kila sehemu
Pamoja na mbwembwe zake zote, Haji Manara alishindwa kufua dafu mbele ya Muro
Wakati wa Muro, Yanga ilikuwa ikishinda nje na ndani ya uwanja
Katika moja ya mahojiano yake hivi karibuni, Muro alisema Yanga inapaswa kurejesha mfumo wa zamani kwa kuwa na mtu ambaye ataitangaza timu hiyo kwa mashabiki
"Tusifananishe Yanga na Simba na timu za Ulaya. Ulaya wana utamaduni wao na sisi katika timu zetu tunao wetu"
"Mtoto wa Manzese ukimpeleka akaishi Masaki hataweza!"
"Utamaduni huo umekuwepo kwa miaka mingi, sisi tumeukuta na tutauacha"
"Kama huyo aliyepewa kitengo Yanga hataki kuongea basi abadilishiwe majukumu, atafutwe mtu mwingine, mbona wapo wengi?," alihoji Muro
0 Comments