Mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba dhidi ya Azam Fc utapigwa Jumamosi, August 17 kwenye uwanja wa Samora
Mwenyekiti wa chama cha Soka mkoa wa Iringa (IRFA) Cyprian Kuyava amesema wanaendelea na maandalizi kuelekea mchezo huo ambao utaashiria ufunguzi wa ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2019/20
Simba imerejea nchini usiku wa kuamkia leo ikitokea Msumbiji ambako jana ilicheza mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo na kupata matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Azam Fc iko Ethiopita ambapo leo itakuwa na kibarua cha mchezo wa kombe la Shirikisho
Simba imetwaa Ngao ya Jamii misimu yote miwili iliyopita kwa kuzifunga Yanga na Mtibwa Sugar
0 Comments