KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa beki mpya wa timu hiyo, Mbrazili, Tairone Santos Da Silva ameanza kujifunza Lugha ya Kiswahili na nyingine wanazotumia wachezaji wenzake.
Hivi karibuni Aussems aliliambia gazeti hili kuwa Da Silva anasumbuliwa na tatizo la mawasiliano kwani hawezi kuzungumza na wachezaji wenzake kwa sababu hajui Kiswahili, Kingereza wala Kifaransa.
Santos ambaye amejiunga na Simba hivi karibuni anajua kuongea Lugha ya Kireno pekee ambayo mabeki wenzake wa kikosini humo hawaijui.
“Santos hawezi kuwasiliana vizuri na wachezaji wenzake kwa sababu hajui kuongea Kiingereza, Kiswahili wala Kifaransa kwahiyo akiwa mchezoni inakuwa ni vigumu kuwasiliana na wenzake.
“Anajua kuongea Kireno tu. Hata hivyo, tayari ameanza kujifunza kuongea Lugha ya Kiswahili ili aweze kuwasiliana vizuri na wachezaji wenzake kwa sababu wachezaji wengi wa Simba wanajua lugha hiyo na baadhi yao wanaongea lugha ya Kifaransa,” alisema Aussems.
0 Comments