Windows

Magari yatakayo tumiwa na viongozi wa SADC yakaguliwa


Serikali imesema maandalizi ya shughuli za SADC yamekamilika kwa kiwango kikubwa na sasa Tanzania iko tayari kuanza kupokea wageni na viongozi waandamizi wa Nchi 16 wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano wa SADC unaofanyika Dar es Salaam Tanzania.


Akizungumza wakati wa ukaguzi wa magari yatakayotumiwa na viongozi mbalimbali watakaohudhuria mkutano huo wa SADC Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi amesema,maandalizi yamekamilika baada ya shughuli ya ukaguzi na kujiridhisha kuhusu utayari wa kuwapokea wageni.

Ameongeza kuwa Serikali imejiridhisha kuwa ina uwezo na iko tayari kuwapokea wageni na viongozi wakiwemo marais wa Nchi 16 za ukanda wa kusini mwa Afrika baada ya kukagua mahali watakapofikia,sehemu ya kufanyika kwa mikutano mbalimbali na mambo mengine muhimu kwa wageni hao.

Aidha, Prof. Palamagamba John Kabudi ameeleza kwa uchache utaratibu wa viongozi wakuu wa Nchi na Serikali watakavyoanza kuwasili kwa kufafanua kuwa marais na wafalme wanatarajiwa kuanza kuwasili Agust 16,2019, licha ya ukweli kuwa shughuli za SADC zimekwishaanza toka August 05,2019 ambayo ilikuwa na wiki ya maonesho ya viwanda na hii leo ni siku ya kilele ambapo Mgeni rasmi wa kufunga maonesho hayo ya viwanda atakuwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mohamed Shein ikifuatiwa na mkutano wa makatibu wakuu,mawaziri na kisha wakuu wa nchi na serikali ikijumuisha Marais na Wafalme.




Post a Comment

0 Comments