UONGOZI wa Lipuli umesema kuwa kwa sasa hauna hesabu za kubeba kombe la Ligi Kuu Bara ambalo lipo mikononi mwa mabingwa watetezi Simba.
Simba ilitwaa ubingwa misimu miwili mfululizo baada ya kuchukua mikononi mwa Yanga msimu wa mwaka 2017/18 na kutetea tena kwa msimu wa mwaka 2018/19.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Lipuli FC, Festo Sanga amesema kuwa mpango mkubwa wa timu ya Lipuli kwa sasa ni kuleta ushindani wa kweli na sio kutwaa kombe.
“Tunatambua kwamba kila timu ina mipango yake nasi pia hatupo nyuma, mpango mkubwa ni kuwa kwenye nafasi nne za juu kisha wakati mwingine tutajipanga kutwaa kombe.
“Kila kitu kinakwenda sawa tunashosubiri ni ligi kuanza ndipo tutaonyesha kile tulichonacho, nafasi ambayo tunaitaka sana ni nafasi ya tatu msimu ujao,” amesema Sanga.
Lipuli FC msimu ujao unaotarajiwa kuanza Agosti 23 itamkosa kocha wao Seleman Matola ambaye kwa sasa anainoa timu ya Polisi Tanzania.
0 Comments