Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ametetea uamuzi wa kumuanzisha mlinda lango Aishi Manula kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 na Simba kutolewa kwenye michuano hiyo
Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kwa Manula kukaa langoni baada ya kuwa nje kwa karibu wiki tatu akiuguza majeraha
Licha ya Beno Kakolanya kuonyesha uwezo mkubwa wakati Manula hayupo, hakupata nafasi ya kuanza mchezo huo
Aussems amesema timu lazima iwe na kipa namba moja, hivyo ulikuwa uamuzi sahihi kumuanzisha Manula kwa kuwa alikuwa amepona
"Lazima tuwe na kipa namba moja, mbili na tatu. Manula alikuwa amepona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua hivyo alistahili kucheza," amesema
Aussems amesisitiza kuwa walinda lango hao watacheza kulingana na utimamu wao kimwili na utayari wa mchezo
0 Comments