Windows

Kauli ya BASATA Kuhusu Tetema ya Diamond Kufungiwa Kenya

BARAZA la Sanaa Taifa (BASATA) limeshangazwa na Serikali ya Kenya kuuzuia wimbo Tetema wa msanii kutoka Tanzania, Rayvanny aliomshirikisha Diamond Platnumz kupigwa kwenye maeneo ya wazi nchini humo.

 

BASATA wamesema wimbo huo ni mzuri kwani hauna tatizo lolote na kawaida yao huwa wanakagua nyimbo zote na kama wimbo ukionekana una matatizo huwa wanachukua hatua ikiwemo kuufungia.

 

“Tumekuwa tukifuatilia nyimbo za wasanii wa hapa nchini na kuwaita wanapokosea. Tunatoa onyo na hata kufungia nyimbo zao, lakini huu (TETEMA) hauna shida ndio maana nasema sijui wametumia vigezo gani kuuzuia usichezwe mchana,” amesema Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza.

 

Wimbo wa Tetema umefungiwa na serikali nchini Kenya kutumika katika maeneo ya wazi kuanzia juzi Agosti 27, 2019, Kwa madai kuwa unamashairi yanayoiharibu jamii hususani watoto.

The post Kauli ya BASATA Kuhusu Tetema ya Diamond Kufungiwa Kenya appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments