

UONGOZI wa JKT Tanzania umesema kuwa kwa sasa kazi imepamba moto kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza Agosti 23 mwaka huu.
JKT Tanzania kwa sasa imejichimbia visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi na mchezo wao wa kwanza utakuwa dhidi ya Simba Agosti 23.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Mohamed Abdalah ‘Bares’ amesema kuwa kikosi kipo vema.
“Kikosi kipo salama na maandalizi yapo sawa kwa kuwa tupo sehemu tulivu mafuzo yanakaa kwenye vichwa vya wachezaji kwa umakini mkubwa.
“Kila mchezaji ana morali kubwa na matarajio yetu kurejea Bara itakuwa kati ya Agosti 20, mashabiki watupe sapoti kwani tunajua mchezo wetu dhidi ya Simba utakuwa mgumu ila tupo tayari,” anesema.



0 Comments