Winga mpya wa Simba Deo Kanda juzi kwenye mchezo kuhitimisha SportPesa Simba Week dhidi ya Power Dynamo, aliwafurahisha mashabiki kwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu
Kanda alijiunga na Simba kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea klabu ya TP Mazembe
Akiwa amekabidhiwa jezi namba 7 iliyokuwa ikitumiwa na Emmanuel Okwi, winga huyo ameanza kwa kupita mulemule kwa Okwi
Kanda juzi alifanikiwa kujitengenezea jina kwa wapenzi wa Simba kutokana na kiwango chake alichoonyesha
Awali wengi waliutilia mashaka ujio wake kunako klabu ya Simba hasa mazingira ya kutolewa kwa mkopo
Hata hivyo kwa kiwango alichoonyesha juzi, Kanda atakuwa mmoja wa wachezaji ambao wataibeba Simba msimu huu
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amemsifia winga huyo kwa kusema anajisikia furaha sana kuwa na mchezaji kama huyo kwenye timu yake
"Ni mchezaji mwenye sifa ya kuichezea timu kubwa Afrika kama Simba, tunafarijika kuwa naye. Kila mmoja ameona uchezaji wake, nadhani atatusaidia kufikia malengo yetu, kwa michuano ya ndani ya na kimataifa,”
0 Comments