HATIMAYE Alexis Sanchez ametua jijini Milan kukamilisha dili la kujiunga na Inter Milan kwa mkopo akitokea Manchester United.
Sanchez ametua jijini hapo baada ya kudumu United kwa miezi 18 akiwa hana mafanikio makubwa lakini bado akiwa na mkataba mrefu na wababe hao wa Jiji la Manchester.
Inaelezwa kuwa Sanchez ataendelea kulipwa sehemu ya mshahara wake na Man United, ambapo Inter imekubali kulipa pauni 4.5m katika pauni 21m ambazo anatakiwa kulipwa na United kwa mwaka mmoja.
Sanchez sasa ataungana na rafiki yake, Romelu Lukaku ambaye tayari ameshatua kikosini hapo na alicheza mchezo wa wiki iliyopita katika Serie A.
The post Hatimaye Sanchez atua Inter Milan appeared first on Global Publishers.
0 Comments