Watu 4 wamefariki dunia na wengine 26, wamejeruhiwa kufuatia ajali iliyohusha basi la abiria na Lori kugongana uso kwa uso katika eneo la nanenane Manispaa ya Morogoro.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo imehusisha basi la abiria lenye namba za usajili T212 DNU na Lori.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa,Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi ambaye alitaka kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua taadhari.
"Ni kweli usiku wa kuamkia leo Ijumaa August 16, saa saba na nusu usiku imetokea ajali eneo la Nanenane, Morogoro, basi mali ya kampuni ya Safari Njema ambayo ilikuwa inatokea DSM kwenda Dodoma imegongana kwa ubavu na lori mali ya Tumbaku Alliance, watu 4 wamefariki.
"Ingawa watu 4 wamefariki ila abiria wengine waliokuwa kwenye basi walikimbizwa Hospitali ya Mkoa Morogoro sababu ya mshtuko na wengi wametibiwa na kuruhusiwa, wamebakia abiria 3 wanaendelea na matibabu, dereva wa lori ni miongoni mwa waliofariki.
"Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa basi ambaye aliovertake pasipo kuchukua tahadhari na kukutana na gari nyingine mbele kisha ajali ikatokea, dereva wa basi ametoweka na tunamtafuta, kama hatopatikana tutamkamata mmiliki wa basi ili atuoneshe dereva alipo". Amesema Mutafungwa
0 Comments