Kampuni ya Oriflame Sweden, imeingiza sokoni vipodozi vipya vya The Novage, vilivyoboresha kuondoa makunyanzi yatokanayo na ongezeko la umri.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuingiza vipodozi hivyo, Meneja wa Oriflame kwa Tanzania, Fortunata Nkya alisema vipodozi hivyo vilivyotengenezwa kwa kutumia viambata asilia vina ubora wa kipekee, kutokana na maboresho yaliyofanywa hivi karibuni.
Alisema bidhaa za the Novage hazitumiii kemikali ya aina yoyote bali inatumia viambata asilia ambavyo havina madhara yoyote kwa ngozi.
“Kwa hiyo katika uasili wake, matokeo yanaonekana haraka kwa kufikia asilimia 40 mara tu unapoanza kuvitumia, bidhaa hizo pia zinatumia mimea ambayo haijarutubishwa kijenetiki (non GMO), kwa hiyo ni za kipekee kwa watumiaji,” alisema.
Alieleza kuwa bidhaa hizo ambazo asili yake hutengenezwa kutoka nchini Sweden ambao wanaaminika kwa kusimamia matumizi ya vitu asilia inaaminika kwa uwezo wake mzuri katika kulinfa ngozi ya mwili na hasa uso, dhidi ya mikunjo na makunyanzi.
“Bidhaa hizi ni kwa ajili ya kulinda zaidi uso. Ziko za aina tofauti katika umri tofauti pia kuanzia miaka 25 na kuendelea, umri ambao ndio hatua za mikunji katika ngozi huanza kuonekana,” alisema Nkya.
Mkurugenzi wa Oriflame Afrika Mashariki, Piyush Chandra alisema aina hii ya bidhaa kwa sasa ipo katika nchi 60 duniani, baada ya kufanyiwa maboresho yanayoendana na wakati huu wa sasa.
“Kwa Tanzania bidhaa hii siyo mpya. Imekuwepo kwa muda mrefu ila sasa tumaifanyia maboresho ambayo niyameifanya kuwa ya kisasa zaidi na yenye matokeo ya haraka,” alisema.
0 Comments