Urusi imeendelea kutuma vifaa vya mfumo wake wa kujilinda na makombora angani chapa S-400 kwenye kambi ya kijeshi iliyopo karibu na mji mkuu wa Uturuki, Ankara.
Tayari ndege tano kati ya sita zinazobeba vifaa vya mfumo huo zimewasili, wakati ndege ya saba ikwa inasubiriwa.
Uturuki itakuwa taifa la kwanza mwanachama wa NATO kuwa na mtambo huo wa kisasa kutoka Urusi.
Uturuki tayari shehena nne za mfumo huo wa S-400 na wamepuuzilia mbali vitisho vya vikwazo kutoka kwa Marekani kwa kununua mfumo huo wa Urusi.
0 Comments