Harry Maguire aweka rekodi ya kuwa mlinzi mwenye thamani kubwa katika historia ya soka baada ya Manchester United kuafikiana na Leicester kumsajili kwa thamani ya £80milioni.
United italipa £60 milioni kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 - ambapo anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya leo Jumatatu, na £20m za ziada zitalipwa siku zijazo.
Leicester inatarajiwa kuijaza nafasi ya Maguire kwa kumsajili mchezaji wa Brighton Lewis Dunk, baada ya kuafikiana kwa mkataba wa thamani ya £45m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.
0 Comments