Janga la njaa duniani kote limeongezeka kwa kasi na zaidi ya watu milioni 820 walikuwa wamekumbwa na janga hilo la njaa mwaka 2018, ripoti ya Umoja wa Mataifa ilisema hapo jana.
Wakati uwiano ulibakia kwa kiasi kikubwa bila kubadilika katika kipindi cha miaka mitatu kidogo chini ya asilimia 11, idadi kubwa ya watu ambao wanakabiliwa na njaa iliongezeka kwa kasi, na kufikia milioni 821.6 mwaka 2018, ripoti iliyozinduliwa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York ilisema.
Ripoti ilitolewa na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF),Shirika la Afya Duniani (WHO), Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo na Mpango wa Chakula cha Dunia.
0 Comments