Mgonjwa wa kwanza wa Ebola mjini Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa DR Congo amefariki dunia.
Gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini Carly Nzanzu amesema, mtu huyu alifariki jana njiani wakati akipelekwa Butembo kwa matibabu kwenye kituo cha matibabu ya Ebola.
Wakati huohuo, Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema, mlipuko wa sasa waEbola nchini DR Congo unaathiri watoto wengi zaidi kuliko milipuko iliyopita.
Msemaji wa UNICEF mjini Geneva Marixie Mercado amesema, hadi tarehe 7 Julai, watoto 750 waliambukizwa virusi hivyo, idadi inayochukua asilimia 31 ya wagonjwa wote wa Ebola, ikilinganishwa na asilimia 20 katika milipuko ya nyuma.
Pia amesema asimilia 40 ya watoto walioambukizwa virusi hivyo wana umri wa chini ya miaka mitano.
0 Comments