Windows

Mazungumzo ya TMC na kundi la upinzani Sudan yaahirishwa tena


Mazungumzo yaliyopangwa kufanyika jana kati ya Baraza la Mpito la Kijeshi la Sudan (TMC) na muungano wa upinzani wa Uhuru na Mabadiliko yameahirishwa tena.

Habari kutoka Shirika la habari la Sudan (SUNA) zimenasema kuwa, mazungumzo hayo yameshindwa kufanyika kwa mara mbili, kutokana na wawakilishi kutoka upande wa kundi la upinzani kutofika.

Habari zinasema, TMC na Umoja wa Afrika hazijatoa taarifa kuhusu kuahirishwa kwa mazungumzo hayo, lakini mmoja wa viongozi wa kundi la upinzani Khalid Omer Yousif amesema kundi lake limetoa ombi kwa Umoja wa Afrika kuahirisha mazungumzo hayo mpaka jumanne.

Post a Comment

0 Comments